Swahili - Sorah Abasa ( He frowned ) - Noble Quran

Noble Quran » Swahili » Sorah Abasa ( He frowned )

Choose the reader


Swahili

Sorah Abasa ( He frowned ) - Verses Number 42
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ( 1 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 1
Alikunja kipaji na akageuka,
أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ( 2 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 2
Kwa sababu alimjia kipofu!
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ ( 3 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 3
Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ ( 4 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 4
Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ ( 5 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 5
Ama ajionaye hana haja,
فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ ( 6 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 6
Wewe ndio unamshughulikia?
وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ( 7 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 7
Na si juu yako kama hakutakasika.
وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ ( 8 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 8
Ama anaye kujia kwa juhudi,
وَهُوَ يَخْشَىٰ ( 9 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 9
Naye anaogopa,
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ( 10 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 10
Ndio wewe unampuuza?
كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ ( 11 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 11
Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ( 12 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 12
Basi anaye penda akumbuke.
فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ( 13 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 13
Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ ( 14 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 14
Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
بِأَيْدِي سَفَرَةٍ ( 15 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 15
Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
كِرَامٍ بَرَرَةٍ ( 16 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 16
Watukufu, wema.
قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ ( 17 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 17
Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ( 18 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 18
Kwa kitu gani amemuumba?
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ ( 19 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 19
Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ ( 20 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 20
Kisha akamsahilishia njia.
ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ ( 21 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 21
Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ ( 22 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 22
Kisha apendapo atamfufua.
كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ ( 23 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 23
La! Hajamaliza aliyo muamuru.
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ( 24 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 24
Hebu mtu na atazame chakula chake.
أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا ( 25 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 25
Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا ( 26 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 26
Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا ( 27 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 27
Kisha tukaotesha humo nafaka,
وَعِنَبًا وَقَضْبًا ( 28 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 28
Na zabibu, na mimea ya majani,
وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا ( 29 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 29
Na mizaituni, na mitende,
وَحَدَائِقَ غُلْبًا ( 30 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 30
Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
وَفَاكِهَةً وَأَبًّا ( 31 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 31
Na matunda, na malisho ya wanyama;
مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ( 32 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 32
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ ( 33 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 33
Basi utakapo kuja ukelele,
يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ( 34 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 34
Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ( 35 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 35
Na mamaye na babaye,
وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ( 36 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 36
Na mkewe na wanawe -
لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ( 37 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 37
Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ ( 38 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 38
Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ ( 39 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 39
Zitacheka, zitachangamka;
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ ( 40 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 40
Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ( 41 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 41
Giza totoro litazifunika,
أُولَٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ ( 42 ) Abasa ( He frowned ) - Ayaa 42
Hao ndio makafiri watenda maovu.

Random Books